PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Maurizio Sarri kataja sababu ya kutompa mkono Pep Guardiola

on

February 10 2019 ulichezwa mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Man City inayofundishwa na kocha Pep Guardiola dhidi ya Chelsea inayofundishwa na Kocha Maurizio Sarri, game hiyo ilichezwa katika uwanja wa Etihad na kushuhudia Chelsea wakiondoka Etihad na kifurushi cha magoli 6-0.

Baada ya mchezo imezoeleka ni kawaida kwa makocha wa timu zote mbili kusalimiana na kupongezana, hiyo ikitafsiriwa kama heshima, upendo na ushirikiano mzuri katika michezo hususani sera za FIFA zinazohusisha kuwa michezo inaendana na vitendo vya kiungwa (Fair Play)

Kocha msaidizi wa Chelsea Zola akiongea na Guardiola na kumwambia kuwa Sarri hakumuona kama anampa mkono.

Mchezo ulivyomalizika Pep Guardiola ambaye timu yake ilikuwa imeshinda magoli 6-0, alikwenda moja kwa moja kumpa mkono kiungwana kocha wa Chelsea Maurizio Sarri lakini hakuupokea mkono wake na baadala yake kuondoka, baada ya mchezo Maurizio Sarri amefafanua kilichotokea.

Kocha msaidizi wa Chelsea Gianfranco Zola alimwabia Pep Guardiola “Hajakuona” baada ya hapo Maurizio Sarri wakati wa Press conference alielezea kuwa hakumuona na ataenda kumsalimia “Sikumuona (Guardiola) kwa wakati ule lakini nitaenda kumsalimia baadae kama kawaida”

“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments