Habari za Mastaa

Zimevuja! Staa wa Marekani anayedaiwa kutoka na Vanessa Mdee kwa sasa

on

Baada ya Vanessa Mdee kuachana na Jux haikuwahi kufahamika kuwa Vanessa anatoka na nani kama ilivyokuwa kwa Jux ambaye alimuweka hadharani mpenzi wake, sasa leo zimeripotiwa taarifa zinazodai kuwa Vanessa Mdee amempata mpenzi mpya ambaye ni staa kutokea Marekani.

Staa huyo wa Bongo Fleva Vee Money amekuwa akionekana akila bata location moja na staa wa Marekani ambaye pia ni mwanamuziki na mwigizaji anayefahamika kwa jina la Rotimi huku wawili hao wakionesha kuwa na ukaribu zaidi kupitia post na komenti ambazo wamekuwa wakiziweka kwenye mtandao wa Instagram.

Hata hivyo moja mtandao maarufu wa mastaa wa huko Marekani “The shaderoom” na wenyewe umeripoti  uwezekano wa kuwepo kwa penzi hilo jipya mjini baada ya kubaini uwepo wa wawili hao kuepo location moja maeneo ya South Beach Miami Florida wakiwa wanakula bata.

 

IMEVUJA!!  MPENZI MPYA WA VANESSA MDEE NI STAA WA MAREKANI..?

Soma na hizi

Tupia Comments