Serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu tofauti na zilizokuwa zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu.
Likwelile amesema ‘kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7 kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha Nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada,chakula pamoja na ruzuku‘.
‘Mkoa wa Dar es salaam imeongezewa shilingi bilioni 2 ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo na kati ya fedha hizo wakufunzi wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio masomoni wametengewa shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli‘
‘ fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Umma , ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko ya hifadhi za Jamii zimetolewa shilingi bilioni 81.13‘
Unaweza kumtazama hapa Katubu Mkuu Dkt. Servacius Likwelile
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE