Top Stories

Update baada ya Freeman Mbowe kulazimika kupelekwa Hospitali jana.

on

hosp 2Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe jana Aug 10 2015 baada ya kumaliza harakati za kumsindikiza Edward Lowassa kuchukua fomu ya Urais kwenye tume ya taifa ya uchaguzi, alipelekwa hospitali baada ya kupata kizunguzungu kikubwa.

Aug 11 2015 baada ya habari kuanza kuenea, aliamua kuwaita waandishi wa habari hospitalini na kuyasema haya yafuatayo >>> ‘ Mimi ni mzima nilipata tu tatizo kidogo jana baada ya msafara mrefu kutokea Buguruni kwenye tume ya taifa ya uchaguzi na hatimaye kuja Kinondoni, nililazimika kuja hospitali sababu ya kuchunguzwa baada ya kukabiliwa na kizunguzungu kikubwa

DSC_0670

James Mbatia, Freeman Mbowe akiwa na Edward Lowassa na mke wake pamoja na Wafuasi wa UKAWA kwenye maandamano jana.

Vipimo vya madaktari kwanza vilinitaka nipumzike kwa saa 48, na majibu ya kiuchuguzi wa kidaktari yakionyesha kwamba nilikua nasumbuliwa na matatizo mawili… kwa kufanya kazi kwa muda mrefu nimekua nikifanya kazi usiku na mchana kutokana na mambo yanayoendelea Tanzania sasa hivi na mwili wa Binadamu una kipimo cha mwisho cha kuchukua adhabu kama hiyo‘ – Mbowe

Kwa kumalizia Freeman Mbowe akasema >>> ‘Ninapozungumza sasa hivi afya yangu ni njema na ninamalizia yale masaa ya mapumziko niliyopewa na Daktari na ndio sababu nilipoona kuna ufatiliaji mkubwa wa afya yangu basi nije tu kuwahakikishia Watanzania wote kwamba niko salama

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments