Mix

FULL VIDEO: Maamuzi ya Waziri Nape baada ya taarifa ya kuvamiwa CloudsTV

on

Leo March 20, 2017 Waziri wa Habari Nape Nnauye amefanya ziara Makao Makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake.

Waziri Nape Nnauye ameunda Tume ya Uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo ambapo pia ametoa masaa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda na kutoa ripoti yake.

Kila kitu kuhusu alichokiongea Waziri Nape Nnauye nimekiweka hapa chini, Bonyez play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments