Habari za Mastaa

Safari ya Pascal wa BSS kwenda kutibiwa India imeiva tatizo Passport

on

Baada ya Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda kumtembelea mshindi wa BSS 2009 Pascal Cassian aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupewa maelezo ya vipimo vya mgonjwa huyo kisha kuahidi kumsaidia kwenda India kwaajili ya matibabu.

Hatimaye leo February 25, 2018 mwimbaji Mrisho Mpoto ametibitisha kuwa tayari mipango yote ya kwenda kumtibu Pascal Cassian nchini India imekamilika licha ya kwamba Pascal amejikuta akipata changamoto ya Passport ya kusafiria.

Hivyo imemlazimu Pascal Cassian kumuomba tena RC Makonda na viongozi mbali mbali waweze kumsaidia ili apate passport itakayo muwezesha kusafiri kwenda India kwenye matibabu.

..>>>“Namshukuru mkuu wa Mkoa Makonda kwa kulibeba hili jambo kama la mtoto wake wa damu lakini changamoto niliyonayo kwa sasa sina Passport mimi na mke wangu, nina omba kwa RC Makonda na Rais Magufuli najua anaona so naomba sana kwa hii serikali pendwa inayosaidia wasiojiweza wanisaidie mimi na mke wangu kusudi niweze kusafirishwa” – Pascal Cassian

Video: RC Makonda alivyomtembelea Pascal wa BSS Muhimbili DSM

VIDEO: Mke wa Pascal Cassian anaeteseka kitandani “msimuache ateseke”

Soma na hizi

Tupia Comments