Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amekutana na Waaandishi wa habari ofisini kwake leo September 5, 2019 na kuwaeleza kuhusu Operation iliyofanywa na Jeshi hilo katika kukabiliana na uhalifu ambapo ameeleza pia kuwashikilia watuhumiwa saba wa biashara ya ukahaba pamoja na kutoa taarifa ya makahaba 15 waliohukumiwa kifungo cha miezi sita kila mmoja.
“Jana mmesikia Mbunge wa viti maalum akizungumzia kuwa kuna makahaba Dodoma, ni kweli na tunawashikilia watuhumiwa saba na pia tumeshawafikisha Mahakamani makahaba 15 na wamehukumiwa jela miezi sita. Hawa badala ya kuwa dada poa wameangukia pua“-Gilles Muroto
BASHE ALIVYOWAACHA HOI WABUNGE KWA MAJIBU YAKE