AyoTV

Kitu Waziri Mwigulu amewaambia Watanzania kuhusu JPM, makinikia (+Video)

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa na kuheshimika hasa katika kipindi hiki cha issue ya mchanga wa madini.

Waziri Nchemba ameyasema hayo akiwa kwenye ziara Jimboni kwake Iramba Magharibi ambapo amewataka Watanzania kuungana na kumuombea Rais ili aendelee na juhudi za kulinda na kusimamia rasilimali za Taifa.

>>>”Kwa imani zetu wote, tuendelee kumuombea Rais wa nchi yetu, Rais wetu mpendwa kwa kazi kubwa anazozifanya ambazo zitasaidi hii mipango mingi tunayopanga kwenye majimbo yetu, matamanio na matarajio yetu mengi tunayokuwa nayo katika majimbo yetu.

“Ukizunguka kote jibu lake linakuja mahitaji ya fedha. Barabara mahitaji ya fedha; elimu bure mahitaji ya fedha, maji mahitaji ya fedha, umeme mahitaji ya fedha, Hospitali huduma bure mahitaji ya fedha. Hicho ndicho kinachomuuma Rais mpaka munaona anachukua hatua ngumu zinazohitaji ujasiri kama anavyofanya.

“Kwa Mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu lazima ataunga mkono juhudi hizo lakini kwa ambaye ana mambo yake ya ubinafsi na ametanguliza ubinafsi anaweza asielewe kazi inayofanywa lakini sisi ambao tunahitaji maji; tunaohitaji barabara, tunaohitaji elimu bure, tunaohitaji Hospitalini dawa ziwepo, tunaohitaji umeme, sote kwa maombi na kwa jitihada na hata kwa kusema tumuunge mkono Rais wetu kwa uzalendo na ujasiri mkubwa aliouonesha.” Mwigulu Nchemba.

VIDEO: “Rais Magufuli amewafanya watu wanachanganyikiwa” – Lucy

Soma na hizi

Tupia Comments