Leo March 6, 2016 Chama cha madereva na makondakta wa daladala Dar es salaam, kimetangaza rasmi kuafikiana na yale makubaliano kati ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na wamiliki wa magari hayo kutoa huduma ya kusafiri bure kwa Walimu wa shule za sekondari kuanzia kesho March 7, 2016.
Ambapo kila mwalimu atatakiwa kuwa na kitambulisho maalum, akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha madereva Tanzania Shabani Mdemu amesema>>
‘Kama Waajiri wetu ambao ni wamiliki wa vyombo vya usafiri walivyolipokea jambo hili na kulipa uzito unaostahiki, vivyo hivyo kwetu Madereva na Makondakta wa mabasi tumeuopokea uamuzi huu kwa namna ya kipekee na tuko tayari kuusimamia na kuutekeleza kwa viwango vinavyotakiwa’
‘Tunatoa wito kwa walimu wote wa Mkoa wa Dar es salaam kuitumia fursa hii waliyoipata bila hofu ili waendelee kutimiza wajibu wao wa kuandaa kizazi bora chenye fikra pevu kwa maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho’
‘Tunaamini kwamba, mchango huu unaotolewa na wadau wa sekta ya usafiri umefungua njia ya mjadala mpana zaidi kuhusu mazingira ya walimu wetu na jitihada zinazopaswa kuchukuliwa ili kuwajengea mazingira rafiki ya kutoa elimu bora kwa watoto wetu’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE