Top Stories

Wafanyakazi 800 wapunguzwa kazini, Mkurugenzi atuma ombi kwa JPM

on

Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza Gypsum cha Lodhia Sailesh Pandit amemuomba Rais Magufuli pamoja na Waziri wa Viwanda kuingilia kati suala la bei ya kununulia malighafi inayotumika katika kiwanda hicho kwa ajili kutengeneza Gypsum za nyumba kwani kwa mwezi wanapoteza zaidi ya Milion 30.

Pamoja na hilo tayari wameshapunguza wafanyakazi zaidi ya mia nane kwa kuwa kiwanda kinashindwa kujiendesha huku akieleza kwamba hali ikiendelea kuwa hivyo kiwanda hicho kitafungwa.

“Kiwanda kinajiendesha kwa hasara tunaiomba Serikali iangalie suala ya ushuru kiwanda kitapata faida na wafanyakazi watakuwa na maisha mazuri na mimi namuunga mkono na najua Rais ataliangalia kwa kuwa ni Tanzania ya viwanda” – Sailesh Pandit

Bonyeza PLAY hapa chini kutazama akielezea..

RC Mongella na Kamati ya Ulinzi na Usalama walivyofanya kazi ya kupasua na kubeba Mawe

Soma na hizi

Tupia Comments