Mix

Pesa zilizokusanywa toka Daraja la Kigamboni lianze tozo zatajwa

on

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii ‘NSSF’ Profesa Godius Kahyarara ameeleza mapato yaliyopatikana kwenye daraja la Nyerere tangu lilipofunguliwa rasmi May 14 2016.

Unaambiwa zimepatikana shilingi Bilioni 1.3 toka tozo mbalimbali zianze kukusanywa kupitia magari binafsi, magari ya abiria, magari ya mizigo, pikipiki na bajaji zinazopita darajani hapo kila siku.

Msimamizi wa mradi wa daraja la Nyerere Gerald Sondo amesema serikali kwa kushirikiana na uongozi wa daraja wanao mpango wa kuboresha huduma za malipo ili watumiaji wa daraja hilo waweze kulipa tozo kwa kutumia kadi za kielektroniki.

Actor Usher Raymond IV poses for photographers upon arrival at the screening of the film Hands of Stone at the 69th international film festival, Cannes, southern France, Monday, May 16, 2016. (AP Photo/Joel Ryan)

Kwa sasa idadi ya magari, pikipiki na bajaji zinazopita darajani hapo ni kati ya elfu 8 hadi elfu 10 kwa siku na wanalipa tozo kulingana na aina ya chombo cha usafiri.

Kuhusu usalama wa daraja na watumiaji wake, Sondo alisema ulinzi ni wa uhakika kwa saa 24 kila siku kwani kuna Askari wa kutosha pamoja na camera zinazosaidia zoezi hilo pia wanaandaa kanuni za matumizi ya daraja ikiwemo faini za uharibifu, uchafuzi wa mazingira, matumizi mabaya ya njia na lugha za matusi.

ULIKOSA HII YA UHARIBIFU KWENYE DARAJA LA NYERERE BAADA YA LORI KUPATA AJALI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments