Duniani

Sheria kali zimechukuliwa baada ya mke kupekua simu ya mumewe bila ruhusa

on

Mke kutumia simu ya mumewe kwa baadhi ya wanandoa inaweza kuwa ni ishu ya kawaida sana lakini kwa Mwanamke mmoja kutoka Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) amelazimika kulipa faini baada ya kukutwa akipekua simu ya mume wake bila ruhusa. Taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo alikua akihisi mumewe kuwa katika mahusiano na mwanamke mwingine.

Mume wa mwanamke huyo alimshtaki kwa kukiuka sheria ya usiri mitandaoni ” na kwamba mkewe alitumia simu yake bila ruhusa na ni kosa. Mwanamke huyo alitakwa kulipa faini ya $41,000 ambazo ni sawa na Milioni 68 za kibongo.

Baada ya kukiri kuwa ni kweli alifanya hivyo kwa kwa kuwa amekua akimuhisi mumewe kuwa na mpenzi mwingine pamoja na faini hiyo mwanamke huyo ameripotiwa kutolewa nje ya nchi kwa muda.

ULIIKOSA HAYA MAMBO MANNE ATAKAYOYAPATA ALIKIBA KWENYE MKATABA MPYA NA SONY MUSIC? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments