Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Jumapili ya February 28 2016 alitangaza kuwa Walimu wa shule za Dar es salaam wataanza kupanda daladala bure kuanzia March 7 2016 baada ya kukubaliana na wamiliki pamoja na madereva wa daladala, habari hii wengine wakaipokea vizuri wengine wakaikosoa.
Dc Makonda amehojiwa na millardayo.com na kusema ‘Najua nipo kwenye jamii ambayo inapenda kuongea sana kuliko kufanya kazi, jamii inayojua kuongelea kukwama kwa jambo hata kabla ya kuanza kufanya kazi , watu wengi wanesema tungewapa pesa ya nauli, wengine wanasema pesa hizi wangepewa wanafunzi, wanasahau kama Walimu ndio uti wa mgongo wa taifa‘
‘Huu ni mchango wa wadau, wadau ndio wanawasaidia Walimu, mimi nasimama kama daraja tu na inabidi watu wajue huu sio mpango wa serikali, ni wadau wamekubali kusaidia Walimu, watu wasichanganye mambo, Mkuu wa Wilaya hana pesa‘ – Makonda
‘Nadhani Walimu walitakiwa kwanza kushukuru wamekumbukwa, ningefurahi wangesema tumepokea nafasi ambayo jamii sasa imeanza kutambua heshima ya Walimu, kwa moyo huu ambao Wadau wameuonyesha tunaiomba sasa wizara ya elimu iendelee kuangalia kuboresha zaidi‘ DC Makonda
Unaweza kuzipata sauti zote za Makonda na Chama cha walimu kwenye hizi video hapa chini…
Hii ndio kauli waliyoitoa Chama cha Walimu kukosoa mpango huo…
Kama ilikupita ya Dc Makonda siku alivyotangaza Walimu kuanza kupanda daladala bure, Hii ndio Video yake…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE