Mix

Maamuzi ya Rais Magufuli kuhusu Mkurugenzi wa jiji Dar es salaam

on

April 19 2016 ni siku ya uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amelizindua rasmi  daraja la Kigamboni na amependekeza liitwe jina la Mwalimu Nyerere na si jina lake kama wengine walivyopendekeza.

Wakati akihutubia Rais Magufuli alimwita mbele Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ili aeleze na awataje kwa majina viongozi ambao wamekuwa wakikiuka sheria, kanuni na taratibu na wanaohusika na vitendo vya matumizi mabaya ya fedha kwenye mkoa wake. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akaeleza vitu vilivyobainika katika stendi ya Ubungo, Makonda amesema…..

>>>‘kwa kutumia by law ya mwaka 2009 inataka kila gari linalotoka Ubungo litumie kulipa sh 8000 lakini tarehe 31 mwezi huo huo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam, Wilson Kabwe akasaini mkataba mwingine unaotumia by law ya 2004 ambayo inaongelea kulipa sh 4000, matokeo yake mkandarasi ana mkataba lakini pia jiji lina mkataba mwingine’ Mkuu wa Mkoa Dar, Paul Makonda

Baada ya Mkuu Mkoa wa Dar es salaam, yakafuata maamuzi ya Rais Magufuli hapohapo ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe…..>>>’na mimi niliapa kusimamia sheria, na mimi viongozi wa namna hii hii ambao wanafaidi jasho la watu wengine kwenye serikali yangu hawana nafasi, kwa hiyo kuanzia sasa Kabwe nimemsimamisha kazi’:-Rais Magufuli

ULIIKOSA YA RAIS MAGUFULI KUTANGAZA KUTENGUA UKUU WA MKOA WA ANNE KILANGO? ANGALIA VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments