Kugundulika kwa gesi nchini kumezidi kuchukua headlines, Mnamo February 24 Serikali ilikuja na habari mpya kuwa gesi imegunduliwa katika bonde la Ruvu mkoani Pwani.
Leo March 15 2016 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ametangaza kuwa gesi iliyogunduliwa bonde la Ruvu ni kiasi cha futi za ujazo trilioni 2.17 na utafiti bado unaendelea. Waziri Muhongo amepata nafasi ya kuzungumza na wanahabari na kutoa tamko la kiasi ambacho kimegunduliwa na kusema…….
>>>’tuna gesi ya kutosha sasa, kwa mfano futi za ujazo trilioni moja tu inaweza kuzalisha megawati 5000 za umeme, ndio maana tunasema ni lazima Taifa letu tuwe na umeme mwingi, wa kutosha na wa bei nafuu, hii iliyogundulika mpaka sasa hivi ni 2.17 sasa tukisema tutumie hiyo trilioni moja tunaweza kuzalisha kiwango hicho cha umeme‘:-Prof. Sospeter Muhongo
Pia amesema utafiti bado unaendelea Ruvu na maeneo mengine ya nchi ambayo yanasadikika kuwa na uwepo wa gesi…..
>>>’huu ni ugunduzi mkubwa ambao utafiti bado unaendelea, huku nchi kavu na baharini bado tunaendelea hasa tunataka kwenda kule kusini zaidi karibu na mpaka wa Msumbiji ambapo nina uhakika tutapata gesi nyingi kama wenzetu wa Msumbiji walivyopata gesi kaskazini mwa nchi yao, kwa hiyo gesi nyingi ipo kusini huko‘:-Prof. Sospeter Muhongo
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA VIDEO YA RAIS MAGUFULI ALIVYOKWENDA BENKI KUU BILA KUWATAARIFU? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI