Wanasayansi wamebaini kuwa malazi ya sokwe mtu ni masafi kuliko ya binadamu ambapo viumbe hao hujenga malazi kwa kutumia matawi na majani ya miti na kulala, moja ya wanafunzi kutoka Marekani Megan Thoemmes, aliongoza jopo na kukusanya sampuli kutoka kwenye Sokwe watu 41 katika bonde la Issa lililopo nchini Tanzania.
Megan Thoemmes alisema kwamba ”Tunajua kuwa makazi ya binaadamu yana aina mbalimbali ya viumbe, mfano, takriban asilimia 35 ya vijidudu kwenye vitanda vya binaadamu vinatoka kwenye miili yetu wenyewe, ikiwemo, kinyesi, kinywani na vijidudu vya kwenye ngozi tulitaka kujua ni kwa namna gani hali hii inaweza kufananishwa na Sokwe hawa,ambao huandaa vitanda vyao kila siku”
Lakini pia watafiti wanasema vitanda vya Sokwe watu ni visafi zaidi kuliko vya binadamu, ingawa viumbe hawa hutumia zaidi ya nusu siku kitandani na kwa malazi ya Sokwe watu nchini Tanzania yana kiasi kidogo cha kinyesi na bakteria kuliko magodoro ya binaadamu majumbani, kwa sababu viumbe hawa huhama wanapolala kila usiku.
Via BBC
Shilole ameingiza tani Moja ya Pilipili zake Sokoni, kafunguka Hapa
Frank aliyenasishwa kiroba cha mahindi ameachiwa huru na Mahakama