Stori Kubwa

Dunia imepata msiba wa mwimbaji wa siku nyingi Prince

on

Legendary wa muziki Marekani na Duniani Prince Rogers Nelson, mwenye umri wa miaka 57 ambaye aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100 na aliwahi kubuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na funk.

Asubuhi ya April 21 2016 Prince amepatikana amefariki dunia katika makazi yake ya huko Minneapolis, taarifa zinasema amekutwa amekwama kwenye lifti katika studio Paisley Park, imeripotiwa kuwa staa huyo inawezekana alikuwa anaumwa kwa kipindi cha muda mrefu ambako kulipelekea hata kulazimika kukatiza Show zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.

Imeripotiwa kwamba wiki iliyopita Staa huyo wa ‘Purple Rain’ alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye show Antlanta Georgia ambapo alilazimisha ndege yake binafsi kutua kwa dharura Molina na alipelekwa hospitali jirani na gari la wagonjwa ambapo alitibiwa na kuruhusiwa masaa machache baadae.

Prince aliwahi kushinda Tuzo za Grammy saba, nyimbo zake tano ziliongoza chart na zingine 14 ziliingia Top 10 pia alishinda Oscar, best original song  ‘Purple Rain’

 PURPLE RAIN, UNAWEZA KUITAZAMA HAPA CHINI

https://www.youtube.com/watch?v=EsRUAoUvP10

ULIMISS YA VITU JOKATE HAPENDI KUONGELEA KWENYE MEDIA, ILE POST YA TYRERSE JE? ANGALIA HII VIDEO HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments