Mix

NEWS: Maamuzi ya Rais Magufuli kwa Mkurugenzi mwingine leo April 28 2016

on

Taarifa ambayo imetoka April 28 2016 ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji ‘TIC’, Julieth Kairuki kuanzia April 24 2016.

Hatua hii imechukuliwa baada ya Rais Magufuli kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo hachukui mshahara wa Serikali tangu alipoajiriwa mwezi April 2013 mpaka sasa, jambo ambalo linazua maswali mengi.

Taarifa hiyo iliyotolewa imesema endapo atakuwa tayari kufanya kazi na Serikali atapangiwa kazi nyingine na Clifford Katondo Tandari atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji.

utenguzi

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB

ULIIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI ALIVYOKWENDA BENKI KUU BILA KUWATAARIFU? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments