Michezo

Thaban Kamusuko akabidhiwa kitita chake

on

Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko aliibuka Mchezaji bora wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Desemba 2015. Mzimbabwe huyo aliibuka baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Amiss Tambwe, raia wa Burundi.

Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Tanzania, wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara jana walimkabidhi kitita cha Tsh Milioni 1 Kamusoko. Kamusoko aliisadia timu yake ya Yanga kupata ushindi katika michezo iliyochezwa mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika mechi tatu zilizochezwa mwezi huo.

Makabidhiano hayo yalifanywa na Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya wakati timu hiyo ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ya Jumamosi dhidi ya APR ya Rwanda Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kamusoko ameishukuru kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kudhamini Ligi Kuu na kumuwezesha kuonesha kipaji chake pia kwa kumkabidhi zawadi ya Fedha. Kamusoko amewashukuru pia mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuwasapoti wachezaji na amesema anawapenda na anawaamini sana.

UNAWEZA KUITAZAMA HII VIDEO HAPA KAMUSOKO AKITOA UJUMBE KWA MASHABIKI

Unataka kutumiwa za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGOandika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard AyokwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Uliikosa video ya magoli yote ya mechi ya  APR Rwanda (1) vs Yanga (2)? Angalia video hii hapa chini  

Soma na hizi

Tupia Comments