Duniani

Mtoto wa mfalme alivyowalipia Mwewe nauli na kuwapandisha Ndege ya abiria

on

Kutoka Saudi Arabia leo mtoto wa mfalme wa nchi hiyo Prince Mohammed Bin Salman ambaye pia ni waziri wa ulinzi ndio anamiliki vichwa vya habari.

Uamuzi wake wa kusafiri na Ndege jamii ya Mwewe wapatao 80 kwenye ndege ya abiria ndio umekua gumzo ambapo ndege hiyo inatajwa kuwa ya shirika la Qatar Aiways. 

Kikawaida ni jambo gumu kuwasafirisha ndege ndani ya ndege tena wanaofikia 80 labda tu uwe mtoto wa mfalmee kama ambavyo Prince Mohamed amefanya hivi karibuni baada ya kuamua kuwalipia nauli mwewe 80 kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 ili kupata siti za ndege hao.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Prince Mohamed inaelezwa kuwa ni kweli kitu hicho kimefanyika na waliwafunga mabawa Mwewe wote ili wasiruke wakati ndege ikiwa safarini.

This picture that appears to show dozens of 'hawks' on a plane has caused a stir on Reddit

Birds of prey can be taken on flights in the Middle East, with airlines including Qatar Airways offering price deals on its website, pictured

Inaelezwa kuwa sio jambo geni kusafirisha wanyama au ndege lakini hawatakiwi kuzidi 6 tu, sasa ili upate ruhusa ya kusafirisha idadi kubwa lazima ulipe fedha nyingi au uwe na kibali maalumu cha viongozi wakuu wa nchi kama ilivyokuwa kwa mtoto wa mfalme.

 VIDEO: Ulipitwa na alichokisema Harmorapa baada ya kuitwa na Mose Iyobo? Nimekuwekea hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments