Mix

Maamuzi ya Dogo Janja baada ya Jux kupata Degree, China (+Video)

on

Mwimbaji staa wa Bongofleva JUX amehitimu Degree ya Computer Science katika Chuo Kikuu cha Guangdong kilichopo Guangzhou, China na baada ya kuost icha zake za graduation ameamsha hisia za mastaa wengi ambao hawakusita kumpongeza.

Miongoni mwao ni mwimbaji staa Dogo Janja ambaye licha ya kumpongeza Jux kwa hatua hiyo hakusita kuelezea kilichopo moyoni mwake kwa kusema anatamani siku moja arudi shule.

“Kwanza napenda kumpongeza Juma Jux kwa kuhitimu masomo yake na ni furaha kuongeza mwanamuziki msomi katika kiwanda cha muziki wa Bongofleva. Ni kitu kikubwa sana.

“Mimi binafsi nimefurahi kwa sababu watu wengi wanatamani kufika kama alipofika Juma especially mtu kama mimi kwa sababu nimekuwa nikitamani kurudi shule. Nimekuwa nikitamani kuona na mimi navaa madude kama yale. So, ni kitu kikubwa sana.

“Kitu nachoweza kusema ni kwamba, muda wowote na saa yoyote pia mi naweza nikarudi shule kwa sababu ni kitu ambacho kinaniumiza sana kwenye maisha yangu nikiona wenzangu kama hivi. Wanafanya muziki, biashara, elimu. Mi niko na vitu viwili tu muziki na biashara lakini elimu ndio kitu ambacho kinamiss katika carrier yangu. So, In Shaa Allah as soon as possible Mwenyezi Mungu akijaalia tunaweza kufanya jambo kwa sababu umri, muda unaenda.” – Dogo Janja.

KAMA ULIKOSA: Kuanzia Jumatatu, usishangae kukosa usafiri wa Daladala ukiwa Mwanza!!

Soma na hizi

Tupia Comments