Watu kumi wakiwemo Walimu saba na Wafanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kuvujisha mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka 2022 kwa njia ya WhatsApp.
Washtakiwa hao ni Patrick Chawawa, Theresia Chitanda, Elinami Sarakikya, Joyce Nkomola , Lloyd Mpande, Olomy Odongo ,Docras Muro na Alcherous Malinzi, Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa serikali Mwandamizi Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Pamela Mazengo.
Inadaiwa kati ya Oktoba 2 hadi 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam washtakiwa, walisambaza mtihani huo kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp na Telegram na kusababisha mtihani huo kuvuja kwa Watu ambao hawakuwa na Mamlaka ya kuusimamia.
Hata hivyo Washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na ni Mshtakiwa mmoja tu ‘Mpande’ ndiye alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana huku wengine wote wakirudishwa Mahaburu, kesi imeahirishwa hadi Novemba 2 mwaka huu.