AyoTV

BUNGENI: Zitto Kabwe, Ester Bulaya na Waitara kuhusu kauli za RC Makonda

on

February 8 2017 Bunge lilipitisha kwa pamoja azimio la kuwaita mbele ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge, Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kutoa lugha za kudhalilisha Bunge.

Baadhi ya Wabunge walisimama kutoa malalamiko yao huku wengi wakiongelea kauli inayodaiwa kutolewa na Makonda huku Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya akidai kupigiwa simu kutoka kwa Makonda yenye kuashiria vitisho dhidi yake, tazama hii video hapa chini kuona wakichangia

FULL VIDEO: Ilivyokua mpaka Wabunge wa upinzani wakatoka nje ya Bunge, tazama kwenye hii video hapa chini

Tupia Comments