Sasa hivi ni rasmi ndege za shirika la ndege la Tanzania (ATCL) zimeanza kusafirisha abiria kati ya Dar es salaam na Dodoma ambapo Waziri Mkuu Majaliwa ndio kazindua safari zenyewe.
“Tuna ndege nzuri, tuzitumie kwenda katika maeneo mengine kwani gharama zake ni nafuu, kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ni sh. 165,000, kwenda na kurudi ni sh. 299,000, ndege nyingine kama hiyo inatarajia kuwasili Tanzania June 2017 na itaongeza idadi ya safari za ndege hizo maeneo mengine ya nchi jirani‘ – Waziri mkuu
Miongoni mwa walioshuhudia ndege hiyo ikitua kwa mara ya kwanza ni pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai, mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Waziri mkuu mstaafu John Malecela ameupongeza uongozi wa serikali ya Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli kwa namna anavyofanya kazi, amefurahishwa na uanzishwaji wa safari hizo.
Kwa upande wake kaimu mtendaji mkuu wa ATCL Captain Richard Shaidi amesema hivi karibuni tunaanza kwenda nchi jirani, mwakani tutapata ndege nyingine kubwa itakayokuwa inafanya safari za masafa ya kati na ya mbali ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Emmanuel Korosso amesema hivi karibuni shirika hilo linatarajia kuanza safari za Tabora, Songea, Mtwara, Mpanda, Mafia na Tanga.
Kuhusu safari za Dodoma amesema zitafanyika mara mbili kwa wiki, siku ya Ijumaa na Jumatatu ambapo hata hivyo wanatarajia kuongeza safari hizo baadae.
ULIPITWA? Askari Magereza wa Tanzania walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Waziri wa mambo ya ndani? bonyeza play kwenye hii video hapa chini