Mkutano wa 6 wa Bunge unatarajiwa kuanza kesho January 31 2017 hadi February 10 2017 Dodoma ambapo Mkurugenzi wa mawasiliano ya Bunge Owen Mwandumbya amezungumza na Waandishi leo Dodoma na kuelezea ratiba kamili ya shughuli za bunge.
Kwa tunavyojua mkutano wa January, February ni mkutano mahususi kwa ajili ya kamati kuwasilisha taarifa zake za utendaji ambapo kipindi hiki kamati 14 za kisekta zitatumia nafasi hiyo kuwasilisha taarifa zake bungeni.
- Tunatarajia kesho kutakua na kiapo cha uaminifu, kitaanza kwa kuwaapisha Wabunge wanne ambapo watatu ni wa kuteuliwa na Rais na mwingine ni wa Zanzibar Ally Juma Ally aliyechukua nafasi ya Mbunge wa Dimani aliyefariki mwaka jana mwishoni.
- Kutakua na taarifa ya Spika na pia kauli mbili za serikali zitawasilishwa bungeni ambapo kauli ya kwanza itahusu hali ya chakula nchini na kauli ya pili itahusu deni la taifa na hali ya uchumi nchini.
- Pia katika mkutano huu tunatarajiwa kuwa na miswada mitatu ya sheria, kama mnakumbuka kwenye mkutano wa 5 wa Bunge uliomalizika November, Miswada mitatu ya sheria ilisomwa kwa mara ya kwanza na kupelekwa kwenye kamati na sasa imeshakamilika.
- Muswada wa kwanza utakua ni muswada wa sheria wa Madaktari wa meno na Wataalamu wa afya shirikishi wa mwaka 2016, Muswada wa pili utakua ni sheria ya huduma ya msaada wa kisheria wa mwaka 2016, wa tatu utakua ni muswada wa sheria ya marekebisho wa sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2016.