Michezo

Gazeti la Sweden limezileta hizi mpya za Zlatan Ibrahimovic!

on

ZlatanLabda hii ni stori nyingine ambayo imewafanya mashabiki wa MLS wafurahie Zlatan kuwa na dalili za kujiunga kucheza ligi ya Marekani ambapo ni fununu zimekua zikienea lakini gazeti moja la Sweden ndio limekolezea wino.

Wino umekolezwa baada ya kuandika kwamba staa huyu ameomba kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini Marekani, yani hajaomba visa ya Utalii, anataka kukaa kwa Obama kabisa.

Gazeti limesema Zlatan alikwenda kwenye ubalozi wa Marekani nchini Ufaransa ambapo pia gazeti hili limerudisha nyuma kumbukumbu za Interview za Zlatan ambae aliwahi kusema anapenda kwenda kucheza soka la Marekani na akamtolea mfano Thiery Henry wakati huo.

Zlatan ambae mkataba wake na PSG ya Ufaransa una uhai mpaka 2016, alisema pia ‘Ni kitu poa sana… na kama nafasi itatokea au kama bado ipo ndani ya miaka miwili au mitatu nitashawishika’

Habari hii imeripotiwa pia na mlssoccer.com pamoja na Sky Sports.

Tupia Comments