Habari za Mastaa

TRACE hawajaichelewesha ya @VanessaMdee !! ni asubuhi mchana na jioni

on

v1Sasa hivi hakuna msanii wa Afrika ambaye hatoshangilia kuona video yake ikichezwa kwenye kituo kikubwa cha TV cha Ufaransa ambacho kimeamua kuweka nguvu zake kwenye kuupa shavu muziki wa Afrika.

Staa wa hit single ya ‘No body but meVanessa Mdee ameongezwa kwenye list ya Watanzania wachache ambao video zao zinaonyeshwa sana Trace Urban ambapo yumo Diamond Platnumz ‘Nitampata wapi‘ Ali Kiba ‘mwana‘ Ommy Dimpoz ‘Wanjera
v 2V Money amevunja rekodi ya video yake hii aliyomshirikisha rapper wa Afrika Kusini K.O kufikia kuonyeshwa mpaka mara tatu ndani ya siku moja kuanzia asubuhi mpaka usiku.

Hiyo ni airtime ambayo yeyote msanii lazima iwe shangwe kubwa manake kituo hiki cha TV kimekua kikikataa kucheza video nyingi tu za Afrika sababu ya kukosa ubora kwenye video na wimbo wenyewe.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments