Mix

Ni kweli ulaji wa kuku wa kisasa unafifisha nguvu za kiume? ninae Daktari mwenye majibu yake hapa

on

HOSPITALSiku zinazidi kusogea, maisha yanazidi kupata ugeni mkubwa wa vitu mbalimbali ambavyo vinakuja kutajwa kitaalamu kwamba ni hatari kwa mwili wa binadamu.

Niko na Mtangazaji aliyetangazwa kushika namba moja Tanzania kwenye maswala ya kijamii Dr. Isack Maro anaesikika kupitia NJIA PANDA ya CloudsFM ambapo kwenye hii post ya leo na anatueleza kuna ukweli gani kuhusu ishu iliyotajwa kwamba kuku wa kisasa ana madhara kwenye mwili wa Mwanaume na anafifisha nguvu za kiume.

Dr. Isaac anaanza kwa kusema >>> ‘Hii ni changamoto ambayo haipo Tanzania peke yake, ulimwenguni ni moja ya changamoto na mjadala mkubwa unaendelea, kuna wale wanatetea haki za walaji na wale ambao wanafanya biashara’

kuku‘Kuku analiwa kuliko mnyama au ndege yeyote duniani, wanasema kwa mwaka kuna kuku milioni 55 ambao wanaliwa zaidi ya ukikusanya pamoja, Mbuzi, Ngo’mbe na Nguruwe’

1. >>> ‘Mbinu ndio zinazoleta madhara, ni mbinu za kisayansi kuhakikisha kwamba kuku anakua na uzito wa kutosha katika kipindi cha wiki tatu, aweze kunona na kuuzika kirahisi’

2. >>> ‘Ukweli ni kwamba kinacholeta madhara sio nyama ya kuku bali ni vile vitu ambavyo vimewekwa kwenye kuku kuhakikisha kwamba kuku huyu anakua, anaongezeka uzito na mengine…….. na bahati mbaya huwa hizi ni kemikali au dawa mbalimbali’

doctor

3. >>> ‘Hizi dawa nyingine sio nzuri kwa mwili wa Mwanadamu hata kwa mwili wa kuku mwenyewe ni vile tu kuku hatumuoni sababu ameshachinjwa’

4. >>> ‘Ili Mwanaume aweze kuwa na nguvu za kiume anahitaji kuwa na uwiano wa kutosha na mzuri katika mfumo wake wa fahamu, wa damu na mwili wake mzima’

5. >>> ‘Moja kati ya vitu vinavyohitajika kwa wingi kwa Mwanaume ni homoni ya kiume ambapo bahati mbaya sana moja ya kemikali zinazopatikana kwa kuku ni homoni zinazomsaidia akue, hizi zikiingia kwenye mwili wa Mwanadamu zinavuruga utaratibu mzima wa mwili kutengeneza homoni, kuna uwezekano mkubwa kabisa ile homoni ya kiume isitengenezwe kwa wingi, hapo ndio tatizo linakoanzia’

Isaack Maro6. >>> ‘Tulizungumzia zamani Wanaume kuwa wanaota vitu kama Matiti, wananenepa kwenye sehemu ambazo hazitakiwi kunenepa kwa sababu ile homoni ya kiume imevurugwa, lakini pia kwa sababu homoni/kemikali tunazomuwekea Kuku ni nyingi kunatokea mvurugano mkubwa kabisa unaovuruga mfumo wa fahamu wa mwili’

Hiyo ni sehemu ya kwanza ya maelezo ya Dr. Isack Maro, sehemu ya pili ya nini cha kufanya itasikika leo Jumatatu April 20 2015 kwenye AMPLIFAYA ya CloudsFM kuanzia saa moja usiku na itapatikana hapahapa on millardayo.com kesho

Msikilize Dr. Isack kwa kubonyeza PLAY hapa chini….

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments