Habari za Mastaa

Wiki isiishe hujaiona hii Episode ya Wema, ndani kuna Penny, Aunt Ezekiel na anaedhaniwa kuwa Mose Iyobo

on

Wema 4In myshoes ni TV show ya Wema Sepetu ambayo huwa inaonekana kwenye TV na baadae inahamishiwa kwenye Internet ambapo kwenye hii ya mwisho kuwekwa YouTube, wanaonekana ndani yake Wema na Ommy Dimpoz walivyokua wakipiga zile picha.

Wengine wanaoonekana ni Aunty Ezekiel ambae alionekana kumlisha keki mwanaume anaedhaniwa kuwa Mose Iyobo, dancer wa Diamond Platnumz anaetajwa kuwa ndio anahusika na unauzito wa Aunty japo Aunty mwenyewe amekua akikanusha.

Kwenye dakika ya 19 ya hii video birthdayboy Martin Kadinda alitaka Mose Iyobo aingie ndani kulishwa keki baada ya kumuona nje ya geiti, Martin alisema ‘kuna yule mwingine nimekuona nae nje, kama ofisi yake haimruhusu mi namtaka aje hapa, si kafika nje?!!!!! baada ya hapo Aunty aliekua akicheka alisema ‘tutalala njaa Martin’

Mwanaume anaeminika kuwa Mose Iyobo aliingia na kumkumbatia Aunty kwa nyuma na kisha kushea keki kwa kulishwa na Aunty mwenyewe.

WemaKwenye hii episode pia anaonekana Penny ambaye ni girlfriend wa zamani wa Diamond Platnumz.

Wema 3

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter Insta FB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments