Stori Kubwa

Imetoka ripoti ya Marais wanaoongoza kwenye twitter Afrika! anaejibu tweets sana je?

on

President 1Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndio Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika akiwa amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Kenyatta ambaye amekuwa madarakani kwa mwaka mmoja amejipatia wafuasi 456,209 na sasa yuko mbele ya mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mwenye wafuasi 408,353 ambae amekuwa mamlakani tangu mwaka 2000 miaka sita kabla hata ya Twitter kuanzishwa.

BBC wamesema Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu ambapo Waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi ‘@AmamaMbabazi,’ ndiye kiongozi anaewasiliana zaidi na wafuasi wake duniani kwenye Twitter huku akiwajibu maswali mbalimbali wanayomuuliza huku asilimia 95 ya mawasiliano yake kwenye Twitter ni ‘@replies,’ yani anajibu maswali ya followers wake.

Uhuru

Uhuru Kenyatta

Utafiti wa kimataifa kuhusu viongozi wanavyojishughulisha na Twitter, wenye mada, Twiplomacy ambapo waziri mkuu mpya wa India Narendra Modi ana wafuasi milioni 4,967,847 na anaelekea kuishinda Ikulu ya white House ambayo ina wafuasi milioni 4,976,734 katika nafasi ya tano.

Zaidi ya asilimia 83 ya mataifa yote duniani yana uwakilishi katika Twitter na asilimia 68 ya viongozi wana akaunti za twitter kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Burson-Marsteller nchini Marekani huku viongozi wanaofuatwa sana kwenye Tiwtter ni pamoja na Barack Obama (@BarackObama) akiwa na wafuasi milioni 43, Papa Francis (@Pontifex) ana wafuasi milioni 14 akifuatiwa na Rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono (@SBYudhoyono) akiwa na wafuasi milioni tano.

Paul Kagame 1Rais Barack Obama alikuwa kiongozi wa kwanza kuanzisha akaunti ya Twitter mwaka 2007 ambapo kati ya serikali 643 zenye akaunti za Twitter ambazo zilitathminiwa katika nchi 161, ni mataifa 32 pekee hasa yaliyo Afrika na Asia ya Pacific ambayo hayana shughuli nyingi kwenye Twitter.

Utafiti huo pia umeonyesha kwamba mawaziri wa mataifa ya kigeni hutumia sana Twitter kutafuta ushirikiano wa kidiplomasia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB

Tupia Comments