Siku chache baada ya Waziri wa Fedha Dr. Philip Mpango atoe agizo kwa vituo vyote vya mafuta nchini kuanza kutumia risiti za kielektroniki (EFD) kila wanapouza mafuta na kufatiwa na agizo lingine kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania juu ya utaratibu huo, zoezi hili limesambaa pia mikoani.
Ripoti kutoka Dodoma zinaeleza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana ameagiza vituo vyote vya mafuta mkoani humo kutumia siku 10 tu kufunga mashine za EFD kwenye vituo vyake na baada ya muda huo kupita watavifungia vituo vyote ambavyo vitakiuka agizo hilo.
RC Dodoma, Jordan Rugimbana ametoa siku 10 kwa vituo vya mafuta mkoani humo kuanza kutumia mashine za kielektroniki EFD kabla havijafungiwa. pic.twitter.com/pA5FBiLlT2
— millardayo (@millardayo) July 16, 2017
VIDEO: TRA wamezungumza kuhusu vituo vya mafuta vilivyofungiwa DSM, Vitafunguliwa? Tazama hapa chini
VIDEO: Waziri wa Fedha alivyofunga kituo cha mafuta Kigamboni. Bonyeza play kutazama