Watu 11 wamefariki dunia wa Kijiji cha Chang’ombe kilichopo Kata ya Segera wilayani Handeni Mkoani Tanga baada ya kugongwa na lori lililokuwa limebeba saruji baada ya kupoteza uelekeo wakati walipojitokeza barabarani walipokuwa wakishanga ajali ya gari dogo aina ya tata .
Watu hao walijitokeza barabarani ili kuweza kutoa msaada kufuatia ajali ya barabarani ya gari dogo aina ya Tata ndipo walipokumbana na ajali hiyo iliyopelekea kupoteza maisha..
Kwa kujibu wa Balozi Dk. Batilda, gari hilo kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, lililobeba abiria ambao idadi yao haijajulika, lilipinduka kwenye kijiji cha Chang’ombe, hivyo wakazi wake na wale wa kijiji jirani Cha Maili Kumi, kwenda kushiriki uokozi.
Wakiwa katika kutekeleza azma hiyo, Balozi Dk. Batilda anasema, ndipo roli hilo likisadikiwa kukata breki, lilipoteza mwelekeo na kwenda eneo waliokuwa wanakijiji wanaokisiwa kufikia 50 na kuwagonga baadhi yao.
Mganga wa Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga – Korogwe, Dk. Paul Patrick amethibitisha kupokea miili ya watu 11 na majeruhi 13.
Amesema hadi kufikia leo asubuhi, miili nane ilikuwa imetambuliwa wakati majeruhi saba wanapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo kwa matibabu zaidi.