AyoTV

UVAMIZI WA KANISA: Mchungaji kaeleza thamani ya vitu vilivyoharibiwa

on

Moja ya story ambayo ilimake headlines siku kadhaa zilizopita ilikuwa ni kuvamiwa na kubomolewa kwa Kanisa la EAGT City Center Mkuyuni Mwanza na kufanywa uharibifu wa vitu mbalimbali.

New story leo July 3, 2017 ni kuwa Mchungaji wa Kanisa hilo Michael Kulola amekaa kwenye EXCLUSIVE interview na Ayo TV na millardayo.com na kaeleza vitu vilivyoharibiwa pamoja na thamani yake akizungumzia pia uhalali wa kuwepo kwenye eneo hilo.

>>>”Thamani ya vitu ambavyo vimeharibika mpaka sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya Tsh. 13m na vitu ambavyo vimeibiwa ni zaidi ya Tsh. 28m. kwa hiyo, thamani kwa ujumla ni zaidi Tsh. 40m ya uharibifu na upotevu.

“Kwa maelezo ya Wapelelezi wamesema jengo ni lazima aje Mthaminishaji kutoka Jiji ili aweze kufanya tathmini na kila kitu aweze kutoa.” – Mch. Michael Kulola. 

VIDEO: Msanii wa Bongo Movie aliyefungua kanisa lake!

 

Soma na hizi

Tupia Comments