Habari za Mastaa

Dancer wa Diamond ameuweka ukweli kuhusu mapenzi yake na Aunty Ezekiel.

on

Screen Shot 2015-05-10 at 9.30.49 AMNi kweli kwamba uko kwenye mapenzi mazito na Mose Iyobo ambaye ni dancer wa Diamond Platnumz? ……………Waandishi wengi walikua wanauliza hili swali kwa Aunty na jibu lake lilikua linaishia kuwa moja tu >>> ‘hata mimi mwenyewe hizo habari nazisikia kama mnavyozisikia nyie, ila baba wa huu ujauzito namjua mwenyewe

millardayo.com imepata nafasi ya kukaa kwenye Exclusive interview na Mose Iyobo anaeonekana mwenye furaha mara nyingi, baada ya kuulizwa kama ni kweli yeye ndio baba Kijacho akaanza kwa kusema >>> ‘Ndio iko hivyo, si unajua mahusiano ni sehemu yoyote hata kwenye daladala yanaanza’

Screen Shot 2015-05-10 at 9.31.11 AMKwenye sentensi ya pili Mose amesema uhusiano wao wa kimapenzi ulianzia wakati wakiwa kwenye tuzo za MTV Durban South Africa June mwaka 2014, walikutana huko na wakajuana huko.

Kwa hivyo tulivyofikia tumekubaliana tu mimi nitakua Baba na yeye atakua mama tuendeleze mwendelezo wa huyo anaekuja‘ – Mose

Hiyo ni sehemu ya kwanza tu ya Exclusive interview, stori kamili itakujia hapahapa millardayo.com siku chache zijazo ambapo ili usipitwe na chochote, jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata iwe usiku au mchana pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Unaweza kumsikiliza Mose akiongea mwenyewe hapa chini..

Soma na hizi

Tupia Comments