Habari za Mastaa

Taarifa kamili ya jinsi Kajala alivyopigwa chupa usiku night club Dar es salaam.

on

kajala 2

May 11 2015 Kajala akionekana na jeraha lake juu ya jicho la kushoto kwenye meza ya Majaji wa shindano la vipaji Kinondoni Dar es salaam.

May 10 2015 mwigizaji wa bongomovie Kajala amekwenda kumsupport msanii Mabeste ambaye alifanya show New Maisha Club kwa ajili ya kuchangisha pesa za kumsaidia mke wake kwenye matibabu.

Kajala anasema >>> ‘Mpaka tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka nikamwambia Meneja wangu amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke, sasa wakati nataka kushuka kwenye gani natembea tu sijui chochote nikashangaa chupa imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringika kwenye zile ngazi, kuna mkaka na mdada wakaniona wakanisaidia’

Kajala 1Aliyenipiga na hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara moja…. amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club nilipelekwa Hospitali Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza, tukarudi Polisi nikaandika maelezo‘ – Kajala

Kwenye sentensi nyingine Kajala amesema ‘Huyu Mwanaume aliulizwa pale Polisi anasema eti ni Pombe, lakini mtu eti Pombe umeingizwa ndani saa moja tu unakumbuka kwamba ni pombe ndio imekufanya hivyo? sio kweli….. itakua tu alidhamiria yeye mwenyewe’

Unaweza kumsikiliza Kajala akiongea yote mengine kuhusu hili tukio kwa kubonyeza play hapa chini….

Ili usipitwe na stori yoyote, jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata iwe usiku au mchana pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments