Mix

Mkenya kwenye headlines za kunyongwa China! safari yake ilikua Nairobi – China.

on

China 2Mwanadada mwenye umri wa miaka 26 huenda akanyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa ya kulevya nchini china ambapo Mkenya huyu Floviance Owino, aliyehudumu kama msaidizi wa nyumbani alitiwa nguvuni May 2013 akisafiri kuelekea Beijing kutokea hapa Nairobi.

Afisi ya ubalozi wa kenya nchini Uchina umethibitisha kwamba huenda Floviance akanyongwa mwaka huu baada ya kifungo chake cha miaka miwili kukamilika na haya maneno ni kwa mujibu wa dada yake ambaye ni Judith Owino.

Judith anasema hakufahamu kuwa dada yake alikuwa amesafiri kwenda China hadi alipopata habari kutoka kutoka ubalozi wa kenya nchini humo.

Mkenya>>Nilifahamu kwa mara ya kwanza kuwa alikuwa China nilipopata simu kutoka kwa ofisi za ubalozi, nlifahamu pia kwamba yuko kizuizini akisubiri kunyongwa, ofisi ya Mashauri ya nchi za kigeni ilinipa habari kuhusu hukumu ya kunyongwa kwa dada na kunipa kibali cha haraka kusafiri kwenda China’

Serikali ya uchina hata hivyo ilimwarifu Judith kwamba alikuwa na muda mfupi kugeuza hukumu hiyo na kuzuia dada yake asinyongwe, walinishauri nitafute wakili hivyo kwa sasa nahitaji visa kwenda china maana mda unazidi kupotea.

Mpaka sasa Judith hajapata fursa ya kuzungumza na Floviance kwani serikali ya china haikukubali hilo lifanyike >>> ‘nilitamani sana kuongea nae lakini walinikatalia, Floviane ana mtoto wa miaka minne aliyemuacha Kenya baada ya kusafiri kwenda China’

Reporter: Julius Kipkoech, Nairobi Kenya.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments