Mix

Maamuzi mapya ya Kenya kwa kila abiria anaetokea Liberia.

on

airport 1Ugonjwa wa Ebola ulikua tishio kubwa na stori inaoongelewa sana kwenye vyombo vya habari hata vya kimataifa miezi kadhaa iliyopita ambapo kwenye nchi kadhaa watu wanaotokea Liberia au nchi jirani zenye ugonjwa huo walipata tabu.

Kenya ilikua imepiga stop abiria wote kutokea Liberia kuingia kwenye nchi hiyo ila sasa kwenye maamuzi mapya serikali ya Uhuru imeondoa marufuku ya muda ya kutowaruhusu hao abiria, wameruhusiwa kuingia kuanzia sasa lakini hata hivyo haimaanishi wataingia tu bila kufanywa chochote.

Kila anaeingia kutoka Liberia  na mataifa jirani yenye ugonjwa huo wataendelea kufanyiwa uchunguzi kila wanapotua hadi ugonjwa huo umalizike kabisa.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments