Habari za Mastaa

Zawadi ya gari kwa Sitti Mtemvu na yake mapya aliyotuletea!

on

Sitti 1Mrembo Sitti Mtemvu zaidi ya wiki moja iliyopita alivileta kwa Watanzania vitu vyake vikubwa ambacho vitaendelea kumuweka kwenye headlines ikiwemo kitabu kiitwacho ‘Chozi la Sitti‘ pamoja na TV show yake ambayo itaanza kuonekana soon kwenye TV na anatarajia kionekane na kwenye DSTV pia.

Walikuwepo watu mbalimbali maarufu wa Tanzania wakiwemo viongozi wa serikali kama Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sophia Simba na Naibu waziri Adam Malima kutoka Wizara ya Fedha ambapo Kitu kingine alichokileta Sitti ni Foundation yake Sitti Tanzania Foundation.

Sitti 2Kwenye mfululizo wa hizi picha pia kuna picha ya gari alilozawadiwa Sitti na wazazi wake….. kwa furaha akaandika ‘Wazazi wangu wamenizawadia gari la mwaka 2015, asante kwa mama na baba

Ni gari ambalo badala ya namba za kawaida limeandikwa jina, utaratibu ambao unaruhusiwa sasa hivi kwa Tanzania ambapo mwanzoni wakati wanatangaza huu utaratibu walisema mwenye kutaka jina badala ya namba kwenye gari atalipia shilingi MILIONI 5 kwa miaka mitatu.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments