BreakingNews

Breaking: Burundi watu wote ndani, Wanajeshi kwa Wanajeshi wanapambana.

on

Breaking‪Kutoka Bujumbura Burundi taarifa za sasa ni kwamba raia wameamriwa kutotoka nje, milio ya risasi inasikika, Wanajeshi watiifu wa Rais wanapambana na waliompindua.

Kingine ni kwamba kituo binafsi cha Radio kilichotumika kutangaza mapinduzi ya Kijeshi kimechomwa moto saa tisa usiku wa kuamkia leo na Wanajeshi wanaomtii Rais, taarifa nyingine kutoka Burundi utazisikia kwenye ‪#‎AMPLIFAYA‬ ya ‪#‎CloudsFM‬ saa moja usiku na pia hapahapa kwenye millardayo.com pindi zinapotokea.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments