Ajali

#Breaking: Mwimbaji Ben Pol anusurika kwenye ajali ya boti iliyozama.

on

SEAMwimbaji Ben Pol staa wa hit single ya ‘Sophia’ amenusurika kifo baada ya boti waliyokua wakisafiria na wenzake kuzimika katikati ya safari.

Baada ya kunusurika na baadae kuokolewa, Ben aliandika maneno yafuatayo kwa herufi kubwa >>> ‘MUNGU MKUBWA NA NINAMSHUKURU SANA KWA KUNIPA NAFASI NYINGINE YA KUISHI DUNIANI, We had a very bad experience today, Tumekaa ndani ya maji kwa zaidi ya lisaa, in the middle of nowhere, baada ya boat tuliyopanda kuingia maji na engine kuzimika, maji yalizidi kujaa , Boat ikazama

Cha kushukuru mungu wengi tulivaa life jackets, na baada ya kukaa majini kwa zaidi ya lisaa ilipita boat ya Wavuvi Wakatuona, Ila kati ya wote tuliyokuwepo kuna mtu mmoja hatujui alipo, na hakuwepo kati ya watu tuliyookolewa, Hawa unaowaona hapa ndio tuliopona, Wanawake watatu, watoto hao walikuwa watatu, wanaume tulikuwa nane, lakini mmoja ndiye hatujui alipo’

Ben Pol kuzama

Hii ni picha aliyoiambatanisha Ben Pol baada ya kuandika hayo maneno kwenye Instagram.

millardayo.com inaendelea kumtafuta Ben kwa ajili ya kujua taarifa zaidi kwenye ajali waliyoipata jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments