Premier Bet
TMDA Ad

Nyumba/ Mijumba

Wachina na balaa zao yani, utakubali kuishi ndani ya ghorofa lililojengwa kwa siku 19 tu? (Pichaz na Video)

on

mini-sky-city-chinaKama unaishi kwenye nyumba yako kabisa labda nianze na hili swali, nyumba yako umeijenga kwa muda gani mpaka imekamilika? Au kama unajenga unatarajia nyumba yako itakamilika kwa muda gani? Kama unahitaji ujenzi wa mjengo wako ukamilike haraka basi unaweza kumpa hilo dili Engineer huyu wa Kichina!!

Zhang Yue amekamilisha kazi ya Ujenzi wa Jengo la Ghorofa lililopewa jina la Mini Sky City  ndani ya China, Jengo hilo lina urefu wa Ghorofa 57 na kazi yote imekamilika kwa muda wa siku 19 tu !!Sky City

Wachina hawana utani, kazi ilipigwa mchana na usiku… Cheki kipande cha hii video uone bwana Zhang alivyosimamia huo ujenzi wake ulioiweka China kwenye headline nyingine !!

Vipi ikitokea unatakiwa kuishi ndani ya mjengo huo utakua na amani mtu wangu?

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments