Mix

Tanzania itazuia matumizi ya dola? Majibu yako kwenye hizi sentensi sita za Waziri Saada Mkuya (Audio)

on

Bureau de Change

Bango la Bureau De Change Dar es Salaam June 01 2015

Mvutano umekuwa mkubwa ndani ya Jengo la Bunge Dodoma kwenye Kikao ambacho Wabunge wamekaa kujadili Bajeti 2015/16, ishu ni kuhusu dola kuonekana imepanda ghafla TZ… Wapo waliopendekeza kwamba Serikali izuie dola isitumike kabisa, Waziri Saada Mkuya alitoa majibu haya jana June 24 2015.

Tuna wasiwasi kwamba kama tutazuia matumizi ya dola, ina maana wengine wanaweza wakachukua dola kwa njia za panya na wakaziondosha hapa nchini.. ni  bora tunajua mzunguko uko kihalali, tutaweka mazingira sahihi kuona dola haiathiri sarafu yetu

mkuya1-640x360

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum

Fedha za kigeni tunazihitaji, sekta ya Utalii ndio inayoongoza kwenye eneo hilo.. kwa sababu kuna vitu vinaingia toka nje hakuna mjadala tunahitaji fedha za kigeni. Hakuna namna tunaweza kuzuia moja kwa moja matumizi ya dola hapa nchini, Serikali itajitahidi kuweka utaratibu ili dola isiathiri shilingi ya hapa Tanzania“>>> Waziri Saada Mkuya Salum.

Msikilize Waziri Saada Mkuya hapa, hii niliirekodi wakati Bunge likiwa LIVE kwenye TV.

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments