Michezo

Mchezaji kamshika mwenzie makalio Ligi ya Copa America, kilichofuatia kikazua utata mwingine !! (Pichaz & Video )

on

redcard

Ligi ya Copa America ni moja ya Ligi za soka ambazo ni maarufu sana duniani, lakini headlines mfululizo ndani ya wiki moja sasahivi sio stori nzuri sasa.. tulisikia kuhusu Shirikisho la Soka Amerika ya Kusini kumpa adhabu ya kusimamishwa mechi nne staa wa soka toka Brazil ambae pia ni winga wa pembeni katika Kikosi cha Barcelona, Neymar  da Silva Santos Júnior.

Leo nimempata huyu mwingine Gonzalo Jara ambaye na yeye kaingia kwenye headlines baada ya kumshika mchezaji mwenzake Cavani skwenye makalio.. inaonekana ni kama haikuwa bahati mbaya kwa vile kabla hajamshika kulitokea kujibizana kati yao.. Video ya tukio hilo imeendelea kusambaa mitandaoni kutokana na hukumu kuonekana kumwangukia asiye na hatia.

Edinson-Cavani-009

Edinson Cavani alikasirishwa na kitendo cha Gonzalo, akampiga kibao cha uso.. refa akatoa kadi ya njano kwa Cavani, lakini kwa vile tayari jamaa alikuwa na kadi ya njano ikabidi apigwe nyekundu na kutolewa nje ya uwanja.

Red Card News

Red Card

Mechi hiyo ilikuwa kati ya  Chile na Uruguay.. wachambuzi wanamjadili Gonzalo bado, wanasema ikitokea Uchunguzi ukaonesha jamaa ni kweli alimshika Cavani kwenye makalio hii itakuwa mara ya pili kwake kufanya kosa linalofanana kabisa na alilomfanyia Luis Suarez mwaka 2013, na mwisho ikawa hivyohivyo Suarez kupiga ngumi ya uso.

Red Full

Unaweza kucheki kilichoendelea hapa.

Tupia Comments