Mix

Kumbe Ebola ilifanya Ndege za Kenya zisitue kabisa Liberia toka 2014 !! Nina ripoti ya Kenya leo.. (Audio)

on

121010-KenyaE1904-01

Kulipuka kwa Ebola Afrika Magharibi ilikuwa ishu ambayo iliathiri nchi nyingi duniani, leo moja ya stori ambazo nimesogezewa kutoka Kenya ni kwamba kumbe Shirika la Ndege la Kenya Airways lilipata hasara ya kama Bilioni 12 kutokana na kusimamisha safari zake kwenda Liberia !

Kenya Airways leo imerudi na taarifa nyingine kwamba wameamua kurudisha utaratibu wa kupeleka ndege zao Liberia kutokana na hali kutulia na Shirika la Afya Duniani kuthibisha kwamba hakuna tena maambukizi ya Ugonjwa huo kwa sasa ndani ya Liberia.

Ndege za Kenya Airways ziliacha kutua Liberia tangu miezi ya katikati ya mwaka 2014.

Stori hiyo nimesogezewa hapa kutoka Radio Jambo Kenya, ukiplay utaisikiliza yote.

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments