Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Haya hapa matokeo ya Liverpool dhidi ya West Brom

on

article-2780469-21F1C71800000578-729_964x386

 

Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika ligi kuu ya England na katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya, washindi wa pili wa ligi EPL msimu uliopita klabu ya liverpool leo walitupa karata yao dhidi ya West Bromwich Albion.

Huku kocha Brandan Rogers akianza kwa kumpiga benchi Mario Balotelli na kumpa nafasi mshambuliaji Rickie Lambert – mabadiliko ambayo yalileta utofauti kidogo kwa Liverpool.

Adam Lallana, ambaye alisajiliwa kutokea Southampton akafunga goli lake la kwanza akiwa na jezi ya Liverpool katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.

Westbrom wakafanikiwa kusawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 56, kabla ya dakika 5 baadae Jordan Henderson kuifungia lIverpool goli la ushindi.

Mpaka mwamuzi Michael Oliver alipopuliza kipenga cha mwisho Liverpool walikuwa wameshinda 2-1.

Tupia Comments