Stori Kubwa

Una mpango wa kwenda Dodoma? Ninayo maneno ya Kamanda wa Polisi hapa.. (Audio)

on

ACP III

Imeandikwa kwenye Magazeti mengi leo July 07 2015 kwamba kama huna shughuli ya kufanya Dodoma, na ulijipanga kwa ajili ya safari ya kwenda huko basi ni bora ukaahirisha ili kuepuka usumbufu.

Ninazo sentensi za Kamanda wa Polisi Dodoma akiagiza haya >>> “Tunaomba kila mmoja atambue na kila mara akumbuke kwamba Ulinzi na Usalama unaanza na yeye mwenyewe kwanza” >>>

ACP II

Jeshi la Polisi linashauri wale wote ambao wanataka kuja Dodoma wiki hii, kama huna shughuli maalum inayomlazimu kuja ni vizuri wasije ili kuepuka usumbufu… Wengine wanaweza wakaja kwa lengo la kushuhudia kinachoendelea au ushabiki tu… Wawaweza wakakosa mahali pa kulala” >>>- ACP David Misime.

Kuna matukio makubwa mawili ndani ya Dodoma wiki hii, Rais JK atavunja Bunge ambalo lilikuwa kwenye Kikao cha Bajeti pamoja na kupitisha Miswada mbalimbali, kingine ni Chama cha CCM kupitisha jina la Mgombea wa Urais kati ya Makada zaidi ya 35 waliojitokeza.

ACP

Sauti niliyomrekodi Kamanda David Misime kwenye Clouds360 @CloudsTV iko hapa.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments