Tuliyasikia mengi kuhusu mfululizo wa matukio ya mashambulizi ya kigaidi Kenya, leo inasikika tena kutoka huko, Shambulio limetokea eneo la Mandera, Kenya.
Watu 14 wamefariki na wengine nane wamelazwa wakiendelea kupata matibabu baada ya Vikosi vya Al Shabaab kuvamia na kufanya Mashambulizi usiku wa kuamkia leo July 07 2015.
Waziri wa Usalama Kenya, Joseph Ole Nkaiserry amesema hakukuwa na taarifa zozote wala dalili za Shambulio hilo kutokea.
Watu waliouawa wengi wao walikuwa wamelala nje ya nyumba zao kutokana na eneo hilo kuwa joto wakati wa usiku.
Story iko yote kwenye hii sauti hapa niliyorekodi Habari ya K24 Kenya.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.