Mix

Kikosi cha Azam FC kimethibitisha kuwapokea hawa watatu toka nje ya TZ..

on

Lukong

Golikipa Nelson Lukong Bongaman, jamaa anatokea Congo ila ni Raia wa Cameroon.

Ligi Kuu TZ bara inatarajiwa kuanza August 2015, Vikosi ya Timu za soka vimeendelea kujipanga na kuimarisha Vikosi vyao ili mambo yaende sawa msimu huu watoke na ushindi, Azam FC wamethibitisha kwamba safari hawako tayari kuukosa pia.

Azam FC jana ilithibitisha kuanza kuwapokea  wachezaji wa kigeni wanaotarajia kujiunga nao na kufanya majaribio na klabu hiyo, kwenye taarifa ya Klabu hiyo imeonesha jana usiku walitarajia kumpokea golikipa ambaye ni raia wa Cameroon, Nelson Lukong Bongaman ambaye alikuwa anachezea timu za Congo DRC.

DSC_0699-af709

Jean Mugiraneza Babtiste

Klabu hiyo ilitarajia pia kumpokea staa mwingine mida ya saa 2 asubuhi ambae ni raia wa Uingereza, Ryan Burge.

Nyota mwingine waliyemtaja kuwa watampokea ni mchezaji kutoka Klabu ya APR ya Rwanda, Jean Mugiraneza Babtiste.

azam+bus

Kikosi cha Azam FC kimeelekea Tanga kwa ajili ya maandalizi ya kukipiga na Klabu ya African Sport kwenye mchezo wao wa kirafiki siku ya Jumamosi katika Uwanja wa CCM Mkwakwani na Jumapili watakuwa na mchezo na Klabu ya Coast Union.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments