Mix

Siku mbili baada ya tukio la Ijumaa, Watanzania hawa 35 Wamefikishwa Mahakamani

on

2Ijumaa kwenye taarifa kubwa kutoka taifa la Tanzania hii ya kituo kidogo cha Polisi Bunju Dar es salaam kuchomwa moto na Wananchi kwa hasira ya Mwanafunzi wa shule ya msingi kugongwa na gari barabarani ilikua miongoni mwa kubwa za hiyo July 10 2015.

3Kwa sababu walitoa malalamiko ya matuta kuwekwa na hayakuwekwa hivyo magari yanapita kwa spidi zote, hasira zao walizimalizia kwa kuchoma moto na kukiteketeza kabisa kituo cha Polisi.

Walifanikiwa kuvunja milango na wakaweka magurudumu na kukichoma moto ambapo wakati wanafanya yote hayo ndani kulikua na mahabusu watatu ambao walitolewa kuokoa maisha yao kabla ya moto kuwashwa.

4Taarifa rasmi za July 13 2015 ni kwamba Waliokamatwa kwa kuchoma moto kituo hicho ni 35 na wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashitaka sita.

6Unaweza kuplay hii video hapa chini ili kuona kituo chenyewe kilivyochomwa moto.

Unahitaji nikutumie kila stori ninayoipata? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments