Moja kati ya habari ambazo zimekuwa zikijadiliwa kwa hivi karibuni ni pamoja na hii ya bandari ya Dar es Salaam kuhusu kubainika kwa makontena 256 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa njiani kusafirishwa kwenda nje ya nchi, siku chache baada ya Rais Magufuli kufanya ziara ya kushitukiza.
Leo March 26 2017 Spika wa Bunge wa Jahmuri ya Muungano Job Ndugai akiambatana na kamati ya bunge ya nishati na madini wametembelea katika bandari ya Dar es salaam lengo likiwa nikutaka kupata ufafanuzi wa kina kuhusu makontena hayo ili bunge kama chombo cha kushauri serikali kuchukua hatua.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Rais Magufuli alibaini makontena 20 yenye mchanga wa dhahabu alipofanya ziara ya kushitukiza lakini baadae mamlaka ya bandari ilibaini makontena mengine 256 yenye mchanga, kitu ambacho kimemshitua spika na kamati ya bunge ya nishati na madini na kuamua kutembelea bandarini.
Ulipitwa na hii? ya Rais Magufuli kusema ‘Unaweza kumchukia mtu lakini usiichukie Tanzania’, Bonyeza play hapa chini kuitazama